Advertisements

Thursday, April 18, 2024

WAZIRI JAFO AFUNGUA MILANGO KWA WADAU WA MAZINGIRA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao na ujumbe kutoka mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali ya The Pew Charitable Trusts (PEW) na Wetlands International (WI) kwa lengo la kuainisha fursa zilizolopo kwenye uhifadhi wa maeneo ya fukwe, Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la The Pew Charitable Trusts (PEW) Bw. Simon Reddy akifafanua jambo wakati wa kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali itaendelea kufungua milango kwa wadau wenye nia ya kuchangia katika hifadhi endelevu ya mazingira.

Amesema hayo wakati wa kikao na ujumbe kutoka mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali ya The Pew Charitable Trusts (PEW) na Wetlands International (WI) kwa lengo la kuainisha fursa zilizopo kwenye uhifadhi wa maeneo ya fukwe, Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.

RAIS SAMIA ATUNUKIWA UDAKTARI WA HESHIMA NA CHUO KIKUU CHA ANKARA UTURUKI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni mbalimbali, viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ankara, mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.

NCHI ZA SADC ZAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAONO YAKE KATIKA USIMAMIZI WA MISITU YA MIOMBO


Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe.Filipe Jaciton Nyusi akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jaciton Nyusi (katikati) akifuatilia mawasilisho kuhusu misitu ya miombo kutoka kwa wawakilishi wa nchi za SADC katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi na Mazingira wa Msumbiji, Mhe.Ivete Maibaze na Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani, Mhe. Hilda Suka-Mafdze (kulia)
Baadhi ya washiriki wa mkutano kutoka nchi mbalimbali wakipiga makofi baada ya kikundi cha burudani cha ngoma za asili kutumbuiza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo uliofanyika jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.

HALMASHAURI YA MPIMBWE YAGUSHI MHUTASARI WA VIKAO WA UPITISHAJI BAJETI



*Kikao cha kugushi walipeleka hazina ajili ya hiyo bajeti
Fedha zilizobadilishwa matumizi bila kuidhinishwa na mamlaka husika na utumiaji wa nyaraka za kubadili matumizi ya udanganyifu kiasi cha Sh. bilioni 4.88

Ukaguzi ulibaini kwamba mamlaka nne za serikali za mitaa zilibadilisha matumizi ya kiasi cha Sh.bilioni 4.88bila kupata idhini kutoka kwa mamlaka husika, zikiwamo Baraza la Madiwani na Waziri wa Fedha.

Halmashauri iliyobanika katika ripoti ya CAG kati ya hizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi ilipanga kutumia bajeti ya kiasi cha Sh.bilioni 7.06 kwa
ajili ya kulipa mishahara hata hivyo, bajeti hiyo ilibadilishwa kwa
kuongeza kiasi cha Sh.bilioni 2.07. Kati ya kiasi kiasi hicho kilichotengwa Sh.bilioni 1.61 tu ndizo zilizotumika.

Pia ukaguzi ulibaini nyaraka za mihutasari ya kikao cha kamati ya fedha, mipango na uongozi kilichofanyika tarehe 5 Juni 2023 zilighushiwa na kuwasilishwa Hazina kwa ajili yakuombakibali cha kubadili vifungu vya bajeti ya mishahara, ingawa kikaohicho hakikufanyika kama inavyoelezwa kwenye.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AMEFUNGUA SKULI YA MSINGI YA HAMID AMEIR DONGE IKIWA NI SHAMRASHAMRA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA.



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Hamid Ameir Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mwakilishi wa Jimbo la Donge pia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed, uzinduzi huo uliyofanyika 17-4-2024.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuendeleza fursa za kuajiri walimu wengi zaidi wa fani zote ili kuondosha changamoto ya walimu Zanzibar.

Dk. Mwinyi ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Hamid Ameir iliopo Donge Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 60 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Alisema, kada ya ualimu ni fani muhimu kuliko zote kwenye sekta za maendeleo, hivyo ameeleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha mazingira bora ya Elimu kwa kuweka sawa mazingira wezeshi ya sekta hiyo pamoja na kuimarisha maslahi ya walimu.

Pia, Rais Dk. Mwinyi ameahidi kuongeza uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya elimu kwa kuipa kipaumbele bajeti ijayo ya sekta hiyo ili kuimarisha mazingira bora kutoka ngazi ya maandalizi, msingi hadi Sekondari na kuimarishwa vituo vya amali pamoja na kujenga dahalia za kisasa kabla ya mwaka 2025.

DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA IMF KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI.


Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Ujumbe wa Tanzania (kulia) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati) wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD) (kushoto), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Bw. Abdelhak Senhadji, akizungumza jambo wakati ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara hiyo, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

BAKIZA YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA CHUO CHA UTAMADUNI KUTOKA URUSI ILI KUIMARISHA MASHIRIKIANO YA KISWAHILI


Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dk.Mwanahija Ali Juma akimkabidhi kitabu cha kamusi sahihi la Kiswahili na utamaduni wa mzanzibar Mwakilishi kutoka chuo cha utamaduni wa Urusi Maria Pateeva wakati alipotembelea Ofisi za BAKIZA kuimarisha mashirikiano, huko Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dk.Mwanahija Ali Juma akipokea vitabu vya Kiswahili vilivyochapishwa nchini Urusi kutoka kwa Mwakilishi wa chuo cha utamaduni wa Urusi Maria Pateeva wakati alipotembelea Ofisi za BAKIZA kuimarisha mashirikiano, huko Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mwakilishi kutoka chuo cha utamaduni wa Urusi Rifat K. Pateev akizungumza na Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Zanzibar DK. Mwanahija Ali Juma wakati alipotembelea Ofisi za BAKIZA kwa lengo la kuimarisha mashirikiano.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar

Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA)limepokea vitabu vya Kiswahili vilivochapishwa na Chuo cha Utamaduni kutoka Urusi ili kuikuza na kuiendeleza lugha hiyo.

MKUTANO WA 10 WA AFIIA WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na Waziri wa Fedha, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) mara baada ya kufungua Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akionesha tuzo aliyokabidhiwa na Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) wakati wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Kushoto ni Waziri wa Fedha Ofisi ya Rais Fedha-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum na kulia ni Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dkt. Zelia Njeza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa tuzo na Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dkt. Zelia Njeza iliyotolewa na Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) wakati wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha na Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) Pamoja na wajumbe wengine wa mkutano.

Wednesday, April 17, 2024

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA MKUTANO WA MAFUNZO KWA TAASISI ZA UKAGUZI NA MABUNGE YA SADCOPAC


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Mafunzo wa Kuwajengea Uwezo Taasisi za Ukaguzi na Mabunge ya (SADCOPAC) unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Uguja Jijini Zanzibar leo 17-4-2024

BAADHI ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati mbalimbali za Bunge wakifuatila hutuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa mafunzo ya kuwajengea uwezo pamoja na ufanyajikazi wa Taasisi za Ukaguzi na Mabunge ya (SADCOPAC) wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akifungua na kuufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 17-4-2024
WASHIRIKI wa Mkutano wa Mafunzo wa kuwajengea uwezo pamoja na ufanyaji kazi wa Taasisi za Ukaguzi na Mabunge ya (SADCOPAC) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo, unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 17-4-2024
BAADHI ya Makatibu Wakuu wa SMZ wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mafunzo wa kuwajengea Uwezo Taasisi za Ukaguzi na Mabunge ya (SADCOPAC) wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 17-4-2024

RAIS SAMIA AWASILI ANKARA UTURUKI KWA ZIARA RASMI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Familia na Huduma za Jamii wa Uturuki Mahinur Ozdemir Goktas mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.

SERIKALI YACHUKUA HATUA KULINDA BEI YA ZAO LA ALIZETI


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali bungeni jijini Dodoma.

Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.
Serikali imesema kuwa imeweka kiwango maalumu cha ushuru wa forodha wa dola 500 za Marekani kwa kila tani moja ya ujazo kwenye mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ili kulinda uzalishaji wa ndani.

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kiteto Mhe. Edward Olelekaita Kisau aliyetaka kujua kauli ya Serikali katika kulinda bei ya zao la alizeti kwa kuongeza kodi kwenye mafuta kutoka nje ya nchi.

Mhe. Chande alisema kuwa Serikali inatoza asilimia 0 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mafuta ya kula yaliyozalishwa nchini kwa kutumia mbegu za mafuta ya kula, ikiwemo mbegu za alizeti ili kuhamasisha uzalishaji.

TANZANIA YAHIMIZA USHIRIKIANO NCHI ZA SADC KATIKA USIMAMIZI WA MISITU YA MIOMBO


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo unaofanyika jijini Washngton DC nchini Marekani leo Aprili 17,2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo unaofanyika jijini Washngton DC nchini Marekani leo Aprili 17,2024.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo unaofanyika jijini Washngton DC nchini Marekani leo Aprili 17,2024.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Deusdedith Bwoyo (kulia) akifuatilia matukio katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo unaofanyika jijini Washngton DC nchini Marekani leo Aprili 17,2024.

SERIKALI YABAINISHA MPANGO WA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI KUZALISHA BIDHAA BORA



NAIBU Waziri wa Viwanda na Biasha, Exaud Kigahe amebainisha mpango wa Serikali katika kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora ili kupata masoko ya uhakika.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Ester Malleko ambaye alitaka kujua mpango wa Serikali wa kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na kupata masoko ya uhakika.

Akijibu swalin hilo, Kigahe alisema Serikali imeweka mipango kadhaa ya kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora ili kupata masoko ya uhakika ikiwa ni pamoja na kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwasaidia wajasiriamali wadogo kupata maeneo/majengo ya kuzalishia bidhaa zao, kuwapatia mitaji kupita Mfuko wa NEDF na nembo ya ubora wa bidhaa zao kwa miaka mitatu bila gharama.

Amesema pia kupitia SIDO, TBS na Wakala wa Vipimo (WMA) kuendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kanuni za uzalishaji wenye tija, elimu ya utambuzi wa vifungashio na ufungashaji bora.

WAZIRI KAIRUKI KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MIOMBO WASHINGTON DC


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Sia Kanza (kulia) alipowasili katika Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani uliopo jijini Washington DC
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akijadili jambo na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Sia Kanza (kulia) alipowasili katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo jijini Washington DC.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani uliopo jijini Washington DC Aprili 15,2024. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Sia Kanza (kulia) na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deusdedith Bwoyo (kushoto).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo utakaofanyika Aprili 16-18 jijini Washington DC Marekani.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha mashirikiano na usimamizi wa misitu ya miombo kwa nchi wanachama za SADC, upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya usimamizi wa misitu ya miombo kwa nchi wanachama wa SADC, namna ya kuhama kutoka matumizi ya nishati chafu kwenda nishati safi pamoja na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mifumo ya ikolojia na uhifadhi wa viumbe hai.

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YAHIMIZWA MKUTANO WA 10 WA WAKAGUZI AFRIKA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akiwataka wakaguzi wa ndani barani Afrika kutumia utaalam wao wa ukaguzi kuzisaidia nchi zao kutatua chamgamoto, wakati wa Mkutano wa 10 wa Wakaguzi wa Ndani Barani Afrika, unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Na. Peter Haule, WF, Arusha.
Wakaguzi wa Ndani barani Afrika wametakiwa kubadilishana uzoefu na kutumia teknolojia katika kutatua changamoto mbalimbali katika taaluma yao na kuhakikisha wanasaidia taasisi na Serikali zao kuboresha ufanyaji kazi ili kuchochea maendeleo.

Hayo yameelezwa jijini Arusha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, wakati wa Mkutano wa 10 wa Wakaguzi wa Ndani Barani Afrika, ulioanza kwa mikutano midogo inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Dkt. Mkuya alisema kuwa mkutano huo umewakutanisha wakaguzi kutoka nchi 27 za Afrika na kwamba mkutano huo ni jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu ambapo wageni watajifunza Tanzania na wageni watajifunza kwa wenzao kwa kuwa mazingira ya ukaguzi yamebadilika kutokana na kuimarika kwa teknolojia duniani.

KIKWETE AWAASA VIJANA KUWA CHACHU YA UTENGAMANO WA KIKANDA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo kabla ya kuhutubia katika mkutano mkuu wa kwanza wa marais na viongozi wa sasa na wa zamani wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uganda ambapo alialikwa kama mgeni rasmi jana Jumatatu.
Makamu wa Rais wa Uganda, Bi. Jessica Allupo akifuatilia hotuba ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano mkuu wa kwanza wa marais na viongozi wa sasa na wa zamani wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uganda.
Wahudhuriaji katika katika mkutano mkuu wa kwanza wa marais na viongozi wa sasa na wa zamani wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uganda ambapo alialikwa kama mgeni rasmi.

CDE. MBETO ATAKA VIWANJA VIWANJA VYA MICHEZO ZANZIBAR VITUMIKE


Na Mwandishi Wetu -Zanzibar.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis,ameishauri Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar kuhakikisha inasimamia vizuri matumizi ya Viwanja vya vya kisasa vya michezo vilivyojengwa na Serikali kwa ajili ya kukuza vipaji vya Vijana kupitia michezo mbalimbali nchini.

Ushauri huo aliutoa wakati akizindua msimu wa nne wa ligi ya mpira wa miguu ya Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Mhe.Ameir Abdalla Ameir "Ameir CUP" iliyozinduliwa katika Uwanja wa Magirisi Unguja.

Amesema Serikali imejenga viwanja vya kisasa kwa kutoa kipaumbele cha kukuza sekta ya michezo nchini.

Katika maelezo yake Mbeto,alisema suala la michezo limepewa nafasi kubwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 ili Wananchi hasa vijana waweze kujiajiri wenyewe kupitia sekta hiyo.

Katibu huyo wa Kamati Maalum Mbeto,alieleza kuwa Wizara ya Habari kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) wanatakiwa kuhakikisha ligi mbalimbali zinazochezwa katika viwanja vya mitaani na zina mashabiki wengi zinachezwa katika viwanja vya kisasa ili kiibua vipaji na kuongeza kipato.

WAZIRI MKUU : MAHAKAMA ZAANZA KUTUMIA MFUMO WA KUTAFSIRI LUGHA ZA KIINGEREZA NA KISWAHILI

*Nia ni kuwawezesha wananchi kuelewa mwenendo wa mashauri

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihitimisha hoja ya bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake, na mfuko wa Bunge kwa mwaka 2024/2025, bungeni jijini Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mahakama zimeanza kutumia mfumo unaonasa sauti na kuzibadilisha kwenda kwenye maandishi huku ukitafsiri lugha za Kiingereza na Kiswahili.

“Hii ni hatua kubwa sana kwani mfumo huo unarekodi sauti na kupeleka kwenye maandishi. Vilevile, unaweza kutafsiri lugha ya Kiswahili au Kiingereza kulingana na uhitaji,” amesema na kuongeza: “Kanuni za Mahakama zimeanza kutafsiriwa sambamba na uandaaji wa mihutasari ya hukumu kwa Kiswahili ili kuwawezesha wananchi kuelewa mwenendo wa mashauri.”

Ametoa kauli hiyo jioni (Jumatatu, Aprili 15, 2024) Bungeni, jijini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2024/2025.

Akielezea mambo yaliyofanyika ndani ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita, Waziri Mkuu amesema mbali ya matumizi ya Kiswahili mahakamani, Serikali imeendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia kutokana na mapinduzi ya nne ya viwanda duniani.

RAIS SAMIA ATOA TANI 189 ZA MBEGU – WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameridhia kutoa tani 189 za mbegu za mpunga, mahindi na alizeti ili zisambazwe kwa wakulima wa wilaya ya Kilombero.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wananchi wote walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazonyesha nchini, lakini pia ametoa mbegu hizo ili kuhakikisha wale waliopata athari katika mashamba yao waweze kuendelea na shughuli za kilimo pale hali itakapokaa sawa,” amesema.
Ameyasema hayo (Jumanne, Aprili 16, 2024) wakati akizungumza na wananchi wa maeneo ya Mlimba, Taweta, Masagati wilayani Kilombero, mkoani Morogoro ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko.

Waziri Mkuu ambaye pia alikagua bonde la mto Kilombero linalojumuisha wilaya tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi, amesema Rais Samia ameelekeza Serikali iendelee kuwahudumia wananchi wote waliopata athari ikiwemo kuimarisha maeneo ya utoaji huduma za afya, kugawa vyakula na kurejesha miundombinu ikiwemo barabara na reli.